Waziri Majaliwa ataka Dar irekebishwe

a

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaka kufanyiwa marekebisho kwa baadhi ya Majiji hapa nchini, ikiwemo ya Dar es salaam, Tanga, na Arusha ili yaweze kuvutia watalii pindi wanapokuwa wanaingia nchini. 

"Lazima tutumie maeneo ya wazi kutangaza vivutio vyetu tulivyokuwa navyo, tukaona jitihada za usafi zikifanyika japo sasa hivi zimeachwa naagiza tuimarishe bustani zetu hapa za Dar." Amesema Waziri Mkuu Majaliwa 

Akizungumza Jijini Dar es salaam Waziri Mkuu Majaliwa amesema si sawa kuona jiji kama la Dar es salaam watali wanaingia nchini halafu Jiji la Dar es salaam linakuwa halifanani kuwa Jiji. 

"Nguzo zote za taa ziboreshwe ziwake usiku ili zipendezeshe usiku kwa wageni wanaoingia usiku, unaingia jijini Dar es salaam jiji liko giza, haiwezekani wametushinda wafanyabiashara binafsi wanatushinda kutangaza juice na Ice Cream halafu sisi hatutangazi utalii." - alisema. 

"Naagiza mikoa na Majiji mengine ambayo iko tayari kuboresha maeneo yao yatakayotumika kwa ajili ya utalii."

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA UDAKU SPECIAL >BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIALLoading...

Waziri Majaliwa ataka Dar irekebishwe Waziri Majaliwa ataka Dar irekebishwe Reviewed by Udaku Special on December 16, 2018 Rating: 5

1 comment:

  1. Mzee ndio kabisa. Halafu biashara ndogo ndogo za aina zote zisiwe barabarani Bali zitafutiwe sehemu maalum. Na nyumba za makazi isiwe kila nyumba mahali pa mifugo au biashara au kiwanda kidogo. Hii inaharibu shoo ya mji. Tutafika tu

    ReplyDelete

Powered by Blogger.