Aunty Ezekiel Ajibu Tetesi Za Kuachana na Mcheza Dancer wa Diamond Platnumz Moses Iyobo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Aunty Ezekiel Ajibu Tetesi Za Kuachana na Mcheza Dancer wa Diamond Platnumz Moses Iyobo
Muigizaji wa Bongo movie mrembo Aunty Ezekiel amefungukia tetesi za Kumwagana na baba Watoto Wake ambaye ni mcheza shoo wa Diamond Platnumz, Mose Iyobo.

Katika siku za karibuni kumekuwa na uvumi mwingi ambao umekuwa ukisambaa kuwa wawili hao hawaonekani pamoja kama zamani kwa sababu Penzi Lao limefika ukingoni.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la DIMBA Jumatano, Aunty Ezekiel amesema kuwa hata ikitokea ameachana na Iyobo itabaki kuwa siri yao Lakini kwa sasa wapo vizuri tu.

Wapo wengi wanaamini sisi hatuwezi kudumu, lakini nataka niwathibitishie kuwa mapenzi yetu yapo salama sana, tumejiwekea mikakati yetu ili kuhakikisha tunaishi kama tunavyotaka na si kama wengine wanavyotaka na hata ikitokea tukiachana naamini itabaki siri ya sisi wawili“.

Aunty Ezekiel amesema moja ya mipango yake kwa sasa ni kuongeza mtoto kwa kuwa ni wakati sahihi kwake na mwenzake kufanya hivyo, kama ambayo walikuwa wamepanga toka awali.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad