Wolper Adaiwa Kumkuwadia Dogo Janja Kwa Demu Mpya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Muigizaji wa Bongo movie Jacqueline Wolper ameibuka na kukana kabisa taarifa zinazodai kuwa amemsaliti rafiki yake Irene Uwoya kwa kumkuwadia shoga yake kwa Dogo Janja.

Dogo Janja ana ‘kifaa’ kingine kipya ambaye ni mtoto mkali, mkazi wa jijini Arusha aliyetajwa kwa jina moja la Linna. Baada ya kusambaa kwa video na picha za Dogo Janja ambaye ni msanii wa Bongo Fleva na Linna wakiwa kwenye mahaba mazito ndipo baadhi ya watu wakaibuka na kila mmoja kuanza kusema lake.



Gazeti la Ijumaa linaripoti kuwa kwa sasa uhusiano wa Uwoya na Wolper hauko sawa. Kufuatia bango hilo kuwa na madai mazito ya Uwoya kupaniki huku Wolper akitajwatajwa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wolper alifunguka na kusema haya:

Kikubwa ninafurahi kwa sababu baada ya kupelekewa hiyo ishu, Irene (Uwoya) hakutaka kuamini kwani ananijua jinsi ninavyompenda na kumchukulia. Anajua siwezi kuwa snichi kwake kwani ninamchukulia kama ndugu yangu. “So hata alivyoambiwa alikuwa ndiye mtu wa kwanza kukataa mimi kufanya hivyo.

Anajua mimi siwezi unafiki ndiyo maana hujawahi kuona nikimposti Dogo Janja (kwenye ukurasa wake wa Instagram) na huyo demu ambaye ni mdogo wangu (Linna) maana nitakuwa mchawi. Yaani mchawi kabisa.

Na mimi ninamlaumu Dogo Janja maana Dogo Janja hajui undugu wangu na Linna kwa hiyo ninahisi alitumia uanaume wake kuni-block (mtandaoni). “Mpaka hapa ninakuambia huyo mdogo wangu, Linna siyo mteja wangu tena na hana tena ukaribu na mimi tangu awe na Dogo Janja.

Sasa nikisema Dogo Janja mchawi nitakuwa mwongo? Mchawi ni mtu mharibifu. “Nilishangaa sana kusikia eti mimi ndiye nimemkuwadia wakati Dogo Janja nilikuwa ninamchukulia kama mwanangu na alikuwa shemeji yangu (kwa Uwoya). “Hiyo skendo ndiyo imenifanya niwakalie kimya Linna na Dogo Janja maana Dogo Janja alikuwa rafiki yangu kabla hata ya kuwa na Irene (Uwoya) na huyo aliyenaye ambaye ni mdogo wangu kabisa.

Kinachoniuma sana ni huo uvumi ulivyotokea maana nilimuuliza huyo mdogo wangu (Linna) na Dogo Janja wakakataa katakata na meseji zao ninazo alafu eti leo hii ninaonekana…. (tusi) wakati Irene (Uwoya) ni rafiki yangu na ni mfanyakazi mwenzangu“.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad