Kanisa Katoliki lasema kuna mshindi wa wazi uchaguzi wa urais

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kanisa Katoliki lasema kuna mshindi wa wazi uchaguzi wa urais
Kanisa Katoliki, ambalo lina ushawishi mkubwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, limesema kuna mshindi wazi wa urais katika uchaguzi uliofanyika Jumapili, kwa mujibu wa matokeo ambao wamefanikiwa kuyaona.

Maaskofu wa kanisa hilo wamewataka watawala nchini humo kuwa wakweli na kutangaza matokeo hayo karibuni.

Kanisa hilo lina maelfu ya wangalizi wa uchaguzi nchini humo na baadhi wamewasilisha ripoti za dosari kadha wa kadha.

Matokeo ya uchaguzi wa urais DRC 'kuchelewa'
Huduma ya intaneti yafungwa DR Congo siku moja baada ya uchaguzi

Tume ya uchaguzi ilitarajiwa kutangaza matokeo Jumapili lakini wiki hii ilidokeza kuwa huenda ikachelewa kufanya hivyo kwani bado haijapokea matokeo kutoka vituo vingi vya kupigia kura nchini humo.

Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (CENI) Corneille Nangaa alisema matokeo ya zaidi ya asilimia 80 ya kura bado yanasubiriwa.

Upinzani pia umelalamikia dosari kwenye uchaguzi huo.

Rais Joseph Kabila anatarajiwa kuondoka madarakani baada ya kuongoza kwa miaka 17 na ameahidi kukabidhi madaraka kwa atakayeshinda uchaguzi.


Kanisa hilo limekuwa likipinga kuongezwa kwa muda wa Rais Kabila madarakani, tangu uchaguzi ulipoahirishwa mara kadha.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad