1/11/2019

Kwa Raha ya Mapenzi Ninayopata Hadi Mikunjo Kwenye Sura Imeniisha- Jay Dee

Kwa Raha ya Mapenzi Ninayopata Hadi Mikunjo Kwenye Sura Imeniisha- Jay Dee
Muimbaji Lady Jadyee kwa sasa anaeeleza kuwa ananawiri kwa jinsi mambo yake yanavyooka kwenye ulimwengu wa mapenzi.

Ni mara chache sana Komando Jide kutoa kauli na kauelezea maisha yake ya kimahusiano yalivyo, hata inavyooneka sasa penzi limeshakuwa kikohozi na kulificha ameshindwa.

"Kupendwa raha bwana,hata mikunjo kwenye sura imeniisha.Nina tabasamu linalo nivisha ujana, kwa raha ya penzi," ameendika Lady Jaydee kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuendelea.

"Nakuona kama maji ya bahari kwenye mwili,huondoa zohari na shari kwa maslah maslahi ya penzi.Nimekuwa mwepesi kwako, kusema nakupenda wewe, kwa hapo zamani hili neno kulisema mpaka niwe high,Kwako nipo huru sijihami, nipo huru," ameeleza Jide.

Hata hivyo Lady Jaydee hajamtaja ni nani hasa anayempa raha hizo kwa sasa, utakumbuka muimbaji
huyo alikuwa kwenye mahusiano na msanii kutokea nchini Nigeria Spicy ingawa siku za hivi karibuni hawajaonekana pamoja kama ilivyokuwa hapo mwanzo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger