1/14/2019

Ndege Ndefu zaidi Duniani yapata Kibali cha Kuanza Matengenezo


Ndege ndefu zaidi duniani yapata kibali cha kuanza matengenezo
Video iliyochukuliwa kutoka kwenye helikopta wakati sampuli ya awali ya ndege aina ya Airlander 10 ilipopaa kwa mara ya kwanza Agosti 2016
Ndege ndefu zaidi duniani ipo tayari kwa ajili ya kuanza kutengenezwa kibiashara na kupakia abiria.

Hatua hiyo inakuja baada ya sampuli ya awali ya Airlander 10 yenye thamani ya pauni milioni 32 - ambayo ni mjumuiko wa ndege na meli inayopaa - kustaafishwa rasmi baada ya kufaulu majaribio ya mwisho.

Kutokana na mafanikio hayo, kampuni iliyobuni ndege hiyo ya Hybrid Air Vehicles (HAV) yenye maskani yake Bedford, Uingereza imepewa ruhusa na mamlaka ya usafiri wa anga wa kiraia wa nchi hiyo Civil Aviation Authority (CAA) kuanza uzalishaji wa aina hyo ya ndege.

Kampuni hiyo awali mwezi wa Oktoba 2018 ilipewa kibali cha usanifu kutoka kwa mamlaka ya usalama wa usafiri wa kiraia barani Ulaya European Aviation Safety Agency (Easa).

Moyo wasahaulika ndani ya ndege
Ndege mpya ya Air Tanzania imetua Dar es Salaam
Haki miliki ya pichaSBNA
Image caption
Airlander 10 baada ya kuanguka Novemba 18, 2017 wakati wa safari ya majaribio
Stephen McGlennan, ambaye ni mtendaji mkuu wa kampuni ya HAV amesema mwaka 2018 ulikuwa mzuri sana na kusema kibali cha Easa kilikuwa ni ishara kubwa.

Amesema kwa sasa azma ya kampuni yake ni kutengeneza ndege aina ya Airlander 10 kwa ajili ya biashara na kupakia abiria.

"Sampuli ya awali imetimiza kazi yake kwa kutusaidia kupata takwimu na taarifa muhimu tulizokuwa tukizihitaji ili kuvuka kutoka hatua ya sampuli mpaka utengenezwaji wa ndege halisi," amesema.

Kwa sasa matarajio ni kwamba ndege ya kibiashara itakamata mawingu ikiwa na abiria waliolipia safari yao miaka ya mwanzoni ya 2020.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger