Mhe. Shonza Atumia Kauli ya Rais Magufuli Kumuonya Gigy Money na Wenzake, Kuhusu Picha za uchi Mitandaoni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Naibu wa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza ameitumia kauli iliyotolewa na Mhe. Rais Magufuli kuwaonya wale wanaotumia mitandao ya kijamii kumong’onyoa maadili hapa nchini.


Kupitia ukurasa wake wa Instagrama Mh. Shonza ameitumia kauli hiyo iliyotolewa na Rais asubuhi wakati wa makabidhiano ya kifaa kitakachotumika katika mawasiliano ambacho TCRA wamekabidhiwa ambapo Rais alisema katika moja ya kauli wakati anaelezea madhara ya mitandao ya kijamii na kusema kuwa “Mitandao ya Kijamii inaleta sana mmong’onyoko wa maadili, TCRA washughulikieni wanaotumia mitandao hiyo kuharibu maadili”


Baada ya kauli hiyo Mhe.Shonza ambaye ni Naibu wa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, yaani Naibu anayeshughulikia mambo yaote yanayohusu habari na mawasiliano ameipost kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusema ” Walengwa natumai ujumbe wenu mmeishaupata kina @gigy_money_ogna wenzio,msidhani hatuwaoni , “ashupazaye shingo yake atavunjika na wala hatapata dawa”


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad