Mtanzania Apata Tuzo Maalumu China, aweka rekodi ya kipekee Afrika

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mtanzania Apata Tuzo Maalumu China, aweka rekodi ya kipekee Afrika
Mtanzania Victoria Mwanziva, amepata tuzo maalumu na utambuzi maalumu kama Mwanafunzi bora katika chuo kikuu cha Harbin Institute of Technology, Mjini Harbin, China ambapo anasoma Shahada ya uzamili yaani Masters in Public Administration.

Victoria Mwanziva amepata tuzo hii ya heshima  akiwa mmoja wa wanafunzi 10 pekee wa Kimataifa waliopewa Heshima Hiyo jimboni hapo na akiwa ni Mwanamke pekee wa kiafrika kuipata tuzo hii.

Mgeni rasmi na aliyekabidhi tuzo hizo ni Mh.Rais wa Chuo cha Harbin , Bw. Zhou (Chancellor Mkuu wa Kampasi zote za HIT China)- aliambatana na viongozi waandamizi wa Chuo hicho na viongozi wa Serikali ya China.

Mwanziva amepata tuzo hii kutokana na mchango wake maswala mtambuka chuoni; kujituma kwake Kimasomo; kupata ufaulu wa juu (Daraja la kwanza).

Victoria Mwanziva anamalizia masomo yake China na kwa sasa anahudumu kama Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Watanzania Nchini China, nafasi hii imempelekea kuimarisha mtandao wa Watanzania wanaosoma China kupitia jumuiya zao za miji wanayosoma.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad