1/11/2019

Mwana FA Awaunga mkono Wakenya Kuupinga muziki wa NigeriaMsanii wa muziki Bongo, Mwana FA ameunga mkono kampeni iliyoanzishwa na wasanii wa Kenya ambapo wanapinga kile wanachoeleza vyombo vya habari nchini humo kucheza zaidi muziki kutoka nje ya nchi hasa Nigeria.

Rapa huyo ameeleza kuwa ni hatua muhimu kwani Wakenya wanapoteza zaidi ukilinganisha na kile
wanachonufaika na muziki huo.

"Kampeni ya wadau wa muziki wa Kenya ni sahihi sana wanafanya kitu sahihi kabisa kuupigania muziki wao," ameeleza.

"Sijawahi kuelewa muziki wa nchi nyingine kupigwa zaidi nchini kwetu kuliko mziki wetu,kwa hivyo nawaelewa, huku pia tulipitia hiyo phase..kufumbia macho masuala ya namna hiyo ni udhaifu wa hali ya juu, mimi naamini kama nchi mnapoteza kuliko mnavyofaidika," amesema Mwana FA.

Ameendeleza kwa kueleza anatumaini kuwa hawatasinzia kwenye kufanya muziki mzuri na hawatazuia moja kwa moija muziki wa nje ya Kenya bali watato nafasi hasa kwa muziki wa Tanzania.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger