1/11/2019

Nilianza Kufanya Wimbo na Papa Wemba Alivyofariki nikaamua Kufanya na Mzee King Kiki- Ay

Nilianza Kufanya Wimbo  na Papa Wemba Alivyofariki nikaamua Kufanya na Mzee King Kiki- Ay
Msanii wa Bongo Fleva, AY ameeleza kuwa wimbo wake mpya, Safari alipanga kumshirikisha msanii kutokea DR Congo, Marehemu Pamba Wemba kabla ya kufariki.

AY ameeleza hayo kwenye mahojiano na kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM ambapo amesema baada ya kifo cha Papa Wemba ndipo akamshirikisha King Kiki.

"Hii kazi ya Safari nilikuwa nifanye na marehemu Papa Wemba lakini wote mnajua mzee wetu alifariki hivyo ikabidi Mzee King Kikiii akae humu" amesema AY.

Msanii wa Tanzania aliyepata bahati ya kufanya wimbo na Papa Wemba enzi za uhai wake ni Diamond Platnumz.

Utakumbuka December 2016 Shirika la habari la Ujerumani, Deutsche Welle (DW) limeripoti kuwa wimbo wa marehemu Papa Wemba, Chacun Pour Soi aliomshirikisha Diamond Platnumz, ndio wimbo uliofunga mwaka kwa kuwa wimbo namba moja katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger