Simba Vitani Leo na As Vita Club Chama Adai Wapo Tayari Kupambana

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Simba Vitani Leo na As Vita Club Chama Adai Wapo Tayari Kupambana
KIUNGO wa Simba, Claytous Chama, ameizungumzia AS Vita Club kuwa ni timu ngumu, lakini watapambana kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo wao wa leo Jumamosi. Chama ambaye tangu hatua ya awali kwenye
Ligi ya Mabingwa Afrika amekuwa akiisaidia kwa kiasi kikubwa timu yake ya Simba, leo Jumamosi anatarajiwa kuwa kwenye kikosi ambacho kitapambana na AS Vita Club ukiwa ni mchezo wa michuano hiyo, hatua ya makundi.



Katika mchezo huo ambao utachezwa kwenye Uwanja wa Martyrs uliopo hapa Kinshasa nchini DR Congo, Simba inatakiwa kuhakikisha haipotezi ili kujiweka vizuri kwenye kundi lake la D ambalo kwa sasa inaongoza ikiwa na pointi tatu.



Chama ambaye ni kati ya wachezaji 19 waliotua jijini hapa Alhamisi kwa ajili ya mechi hiyo, alisema: “Mechi itakuwa ngumu kutokana na wapinzani wetu kuwa nyumbani kwao, lakini licha ya sisi kuwa ugenini, hatutakuwa wanyonge.



“Tupo tayari kwa vita, tutapambana nao mwanzo mwisho kuhakikisha
hatupotezi mchezo huu, tumedhamiria kufika mbali, hivyo ni lazima kulinda kila pointi kwenye mechi zetu. “Niseme tu, kwa muda ambao tumekaa huku DR Congo, tayari tumezoea hali ya hewa na mazingira yake, hivyo tupo vizuri.” Simba ilitua hapa DR Congo juzi Alhamisi na inatarajiwa kurejea Tanzania kesho Jumapili baada ya mchezo huo kuchezwa leo Jumamosi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad