1/14/2019

Tundu Lissu Apigiwa Kampeni ya Urais


Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Jesca Kishoa amesema zawadi pekee ambayo Watanzania wanaweza kumpa mbunge wa chama hicho jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu ni kumuunga mkono katika ndoto zake za kugombea urais mwaka 2020.


Kishoa ametoa kauli hiyo leo Januari 14, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali kuhusu afya na maendeleo ya Lissu.

“Lissu ni kaka yangu, ni mbunge mwenzangu na kiongozi wangu, mambo ya kuangalia ni kupata baraka za chama lakini anafaa,” amesema Kishoa.

Amesema wakati ukifika atatamani kuona jina la Lissu likipitishwa kuwania urais, kwa kuwa Watanzania wanajua msimamo wa kiongozi huyo na ndio anayefaa kuwaongoza.

Lissu kwa sasa anaendelea na ziara yake kwenye nchi za Ulaya na marekani kwa ajili ya kuelezea mkasa wa kupigwa risasi uliompata Septemba 2017 Jijini Dodoma.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

2 comments:

 1. Ili aiuze nchi yetu?!
  Anatumika ujue!!

  ReplyDelete
 2. Aiuze mara ngap ?????
  Mbona ilishaga uzwa kitaaaambo??????

  Labda ailipie deni il tuwe huru.


  Hata kama akitumika ni bora kuanza nae...kuliko kucha...

  ReplyDelete

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger