Zari Afunguka Kuhusu Mbadala wa Diamond

Zari Afunguka Kuhusu Mbadala wa Diamond
MWANAMAMA Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ juzi kati alifungukia mwanaume atakayechukua nafasi ya mzazi mwenzake, Nasibu Abdul ‘Dia­mond’ na kudai kuwa si mwanaume anayependa mitandao ya kijamii.  Zari alifikia hatua ya kuweka wazi hayo alipoulizwa kama kweli hana mpango wa kuolewa na Diamond na atamuanika lini mwanaume anayempenda am­bapo alieleza kuwa mwanaume wake si wa mitandao ya kijamii.

“Mume wangu siyo wa social media, ni mume wangu siyo wetu,” aliandika Zari alipomjibu shabiki mwingine aliyem­wambia atafute mwanaume wa kuzeeka naye. Baada ya majibu hayo Ijumaa Wikienda lilimsikia rafiki mmoja wa Diamond (jina linahifadhiwa) anayei­fahamu vizuri familia hiyo akidai kuwa siku nyingi Zari ana mwanaume anayetoka naye kimapenzi lakini hapendi kuweka wazi kwa sababu mwanaume huyo amemzuia.

“Zari siyo kwamba hana mwa­naume tangu aachane na Diamond na si kama hapendi kumuonesha, anapenda sana lakini unaambiwa mwanaume huyo hapendi mambo ya mitandao ya kijamii kwani ni mtu mwenye heshima zake,” alisema rafiki huyo wa karibu ambaye aliomba hifadhi ya jina lake.

TUJIKUMBUSHE

Zari ambaye ana watoto watano wawili kati yao amezaa na Diamond baada ya kuachana na Mbongo Fleva huyo amewahi kuhusishwa kimapen­zi na mwanaume anayeitwa Brian wa nchini Uganda ambapo mara mbili to­fauti alionekana kupiga naye picha za ukaribu lakini mwenyewe alidai kuwa ukaribu wao huo ni wa kikazi tu.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA APP YA UDAKU SPECIAL BONYEZA HAPA  

Loading...

Zari Afunguka Kuhusu Mbadala wa Diamond Zari Afunguka Kuhusu Mbadala wa Diamond Reviewed by Udaku Special on January 14, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.