Baba Diamond Alia Kukosa Ushirikiano Kutoka Kwa Familia Yake

Baba Diamond Alia Kukosa Ushirikiano Kutoka Kwa Familia Yake
Baba mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Abdul Juma amefunguka na kusema kuwa yeye na Familia yake wamebaki kuwa jina tu Lakini hawana mahusiano.

Baba Diamond amefunguka machungu yake Baada ya kuona Jinsi Diamond mama yake na Dada yake wanavyoishi maisha ya raha huku yeye ambaye ni baba alitaabika hasa Baada ya kuona Diamond amehamia kwenye mjengo wake mkubwa.


Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Baba diamond amefunguka haya:

Unajua mimi na ile familia siyo kitu kimoja kabisa, nimeona kwenye mitandao ya kijamii wakila bata kwenye mjengo mpya aliohamia Diamond huku akiwa na mpenzi wake mpya huyo Tanasha (Donna), lakini mimi sikupewa mwaliko wowote ule, lakini hata hivyo hili jambo halinipi shida kabisa kwa sababu hivi sasa mimi na Diamond limebaki jina tu, yaani mimi najua kama nina mtoto anaitwa Diamond na yeye anajua kuwa ana baba ambaye ndiye mimi, lakini hatushirikishani kwenye mambo yetu”.

Kwa miaka mingi Diamond amekuwa hana mahusiano mazuri na baba yake huyo ambaye amwshawahi kukiri kuwa aliwahi kumuacha wakati mdogo.HABARI HIZI ZINAPATIKA UDAKU SPECIAL APP BONYEZA HAPA UWE NAYO KWENYE SIMU YAKO

Loading...

Baba Diamond Alia Kukosa Ushirikiano Kutoka Kwa Familia Yake Baba Diamond Alia Kukosa Ushirikiano Kutoka Kwa Familia Yake Reviewed by Udaku Special on February 11, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.