Kwa Tanzania Simba ni Alpha na Omega- Haji Manara

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kwa Tanzania Simba ni Alpha na Omega- Haji Manara
Baada ya kumalizika kwa mchezo wa jana, Jumanne wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya African Lyon na Simba, Kocha wa African Lyon, Suleyman Jabir amesema kuwa Simba ilibebwa kupata matokeo.


Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, imeshuhudiwa Simba ikiitandika African Lyon kwa mabao 3-0, ambapo baada ya kocha Jabir kulalamikia maamuzi ya uwanjani, Afisa Habari wa Simba, Haji Manara akaibuka na kujibu tuhuma hizo.

Manara amesema, "hayo maneno ya kubebwa ni ya kawaida, hata Yanga walisema, kila timu inasema, basi tufanye kila timu iwe inakuja na makocha wake na madaktari wake ndio wawe waamuzi kwasababu hizi lugha za kihuni".

"Tatizo la watu wanaaminishana mambo ya kubebwa bebwa, Simba ina uwezo wa kimpira kuliko klabu yoyote Tanzania kwahiyo yoyote atakayekuja ataona anaonewa tu. Kwa 'level' ya Tanzania sisi ni Alpha na Omega", ameongeza Manara.

Baada ya mchezo huo sasa Simba inarejea Jijini Dar es salaam kwaajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya 'Wana lambalamba' Azam FC utakaopigwa Ijumaa, Februari 22.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu Hajji ndo maana uwa anatukanwa halafu anasema anabaguliwa kwa ulemavu wake. Hivyo alivyo anachonga, Je Angekuwa Kama Wambura ingekuwaje? Aaminiki huyo aliisha waliza chama tawala huyo.

    ReplyDelete

Top Post Ad