Mbunge Chadema Anusurika Kifo Baada ya Kupata Ajali Mbaya Dumila Morogoro

Mbunge Chadema Anusurika Kifo Baada ya Kupata Ajali Mbaya  Dumila Morogoro
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimethibitisha Mbunge wake wa viti maalum kutokea Zanzibar, Zainab Mussa Bakari kupata ajali katika eneo la Dumila mkoani Morogoro alipokuwa akitokea Jijini Dodoma kuja Dar es salaam kufuatia kuahirishwa kwa vikao vya Bunge.

Taarifa ya ajali hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CHADEMA, Tumaini Makene akisema kuwa Mbunge huyo anatarajiwa kuhamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.

"Mbunge wa CHADEMA (VM) Zanzibar, Bi. Zainab Mussa Bakari amepata ajali eneo la Dumila akitoka Dodoma leo, abiria wote 3 na dereva wamejeruhiwa."

"Baada ya kutibiwa kwa dharura Morogoro, sasa wanapelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi na matibabu zaidi" ameongeza MakeneHABARI HIZI ZINAPATIKA UDAKU SPECIAL APP BONYEZA HAPA UWE NAYO KWENYE SIMU YAKO

Loading...

Mbunge Chadema Anusurika Kifo Baada ya Kupata Ajali Mbaya Dumila Morogoro Mbunge Chadema Anusurika Kifo Baada ya Kupata Ajali Mbaya  Dumila Morogoro Reviewed by Udaku Special on February 11, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.