Mkurugenzi Anayedaiwa Kuua Kanisani Atoa Mpya, Adai Anasingiziwa, Waumini Walioshuhudia Wampinga


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, Pius Luhende anayedaiwa kuhusika na mauaji ya Isaka Petro kanisani, ameita tukio hilo ni la kupakaziwa tu.

Mkurugenzi huyo ni miongoni mwa watu saba wanaoshikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo yaliyotokea Jumamosi iliyopita katika Kanisa la Wasabato Kijiji cha Kazikazi mkoani humo.

Taarifa ya Polisi inasema kuwa Luhende alipoingia ndani ya kanisa hilo ilitokea vurugu na akaamua kutoka nje kabla ya askari wanyamapori waliokuwa na silaha kufyatua risasi kadhaa na moja ikampiga Isaka na kufariki dunia papo hapo.

Hata hivyo, waumini waliokuwepo katika kanisa hilo wakati mauaji hayo yakitokea wamepingana na polisi wakisema kuwa mkurugenzi huyo ndiye alimfyatulia risasi Isaka.HABARI HIZI ZINAPATIKA UDAKU SPECIAL APP BONYEZA HAPA UWE NAYO KWENYE SIMU YAKO

Loading...

Mkurugenzi Anayedaiwa Kuua Kanisani Atoa Mpya, Adai Anasingiziwa, Waumini Walioshuhudia Wampinga Mkurugenzi Anayedaiwa Kuua Kanisani Atoa Mpya, Adai Anasingiziwa, Waumini Walioshuhudia Wampinga Reviewed by Udaku Special on February 09, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.