Mwigulu Nchemba aeleza sababu za ukimya wake

Mwigulu Nchemba aeleza sababu za ukimya wake
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema kwa sasa amekuwa kimya kutokana hayopo tena kwenye nafasi hiyo, hivyo amekuwa na vitu vichache vya kusemea.

Ameeleza hayo kwenye mahojiano na kipindi cha Clouds 360 kinachoruka Clouds TV amesema kwa sasa amekuwa zaiddi jimboni kwake.

"Unajua ukiwa kwenye nafasi ya uwaziri vipo vitu vingi vya kuvisemea, ndio maana sasa hivi nipo kimya nimebaki na vitu viwili tu vya kusemea mambo ya jimboni kwangu na kazi nzuri inayofanywa na serikali yangu," amesema Dkt. Mwigulu.

Ameendelea kwa kusema, 'Hakuna tofauti na maisha yangu hayajabadilika, nilipokuwa waziri kwenye msafara wangu sikutaka magari yasimamishwe ili nipite, kwa sababu kuna wengine walikuwa wanawahi ndege "airport', wengine wagonjwa na wengine makazini sikutaka kuwachelewesha,'.

Utakumbuka July 2018 Rais John Magufuli alifanya mabadiliko madogo katika baraza lake la Mawaziri, ambapo ameteua Kangi Lugola (aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira), kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Mwigulu Nchemba.HABARI HIZI ZINAPATIKA UDAKU SPECIAL APP BONYEZA HAPA UWE NAYO KWENYE SIMU YAKO

Loading...

Mwigulu Nchemba aeleza sababu za ukimya wake Mwigulu Nchemba aeleza sababu za ukimya wake Reviewed by Udaku Special on February 11, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.