Piere wa Liquid AREJESHA Furaha ya Ommy Dimpozi..Nilipokuwa Naumwa Alinibariki Sana

Piere Likwidi arejesha furaha ya Ommy Dimpozi

Mwanamuziki Omari Nyembo, 'Ommy Dimpozi ameeleza kwamba katika kipindi alichokuwa akijiuguza maradhi yaliyokuwa yakimkabili tangu mwaka jana,alikuwa akifurahishwa na waigizaji wa komedi kwa kutazama video zao.

Kupitia mtandao wake wa Youtube, katika mahojiano maalumu Dimpoz amesema wakati alipokuwa akitazama video hizo wakati mwingine alikuwa akisahau matatizo yake ya ugonjwa.

Yupo huyu jamaa, anaitwa Piere Likwidi. Yaani kila nilikuwa nikimtazama nacheka sana. haswa ile staili yake ya kuongea...Mamaa.....Aiiii...nakufaa.. Kuna siku nilicheka mpaka daktari wangu kule Ujerumani akaniuiza mbona unacheka nikamwambia ni mambo ya Tanzania hawezi kuelewa.

Ommy ameongeza kwamba mbali na Piere ambaye alipata umaarufu mitandaoni, ameeleza pia kuwa makomediani wa tanzania walikuwa wakimpatia furaha na wengine kutoka Kenya.

Amefafanua kilichokuwa kikimfanya asisikilize sana muziki ni kuwa aliogopa kukufuru Mungu kwani roho ilikuwa ikimuuma akijiangalia yupo kitandani huku wenzake wakiwa wanaendelea na kazi. That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments