google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Rais Magufuli Ateua Wakurugenzi na Mwenyekiti | UDAKU SPECIAL

Rais Magufuli Ateua Wakurugenzi na Mwenyekiti

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais Magufuli Ateua Wakurugenzi na Mwenyekiti
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 19 Februari, 2019 amemteua Bw. Hosea Ezekiel Kashimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (Public Service Social Security Fund - PSSSF).

Bw. Kashimba anachukua nafasi ya Bw.  Eliud Sanga ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Kashimba alikuwa Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa Shirika la Hifadhi ya Jamii la NSSF.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi wengine 2 kama ifuatavyo;

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Augustine Emmanuel Mbokella kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Biashara ya TIB (TIB Corporate Bank Limited).

Na pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Latifa Mohammed Khamis kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Biashara za Nje (TANTRADE).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hawa umeanza leo tarehe 19 Februari, 2019.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad