WIMBO wa Tetema wa Rayvanny na Diamond yatoa Marekani


Msanii wa muziki kutoka nchini Marekani, Kevin Gates ameonyesha kuukubali wimbo mpya wa
Rayvanny na Diamond Platnumz unaokwenda kwa jina la Tetema.

Mkali huyo aliyetamba na ngoma '2 Phones' ameweka video kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonyesha akisikiliza wimbo huo akiwa kwenye gari lake.

Wimbo Tetema ulitoka wiki iliyopita na video yake ikatoka hapo juzi ambapo iliweza kufikisha watazamaji (views) Milioni 1 ndani ya saa 17 pekee kwenye mtandao wa YouTube na kuwa wimbo wa kwanza kwa Rayvanny kufanya hivyo.

Hata hivyo Rayvanny ameshindwa kuifikia rekodi ya Diamond kupitia wimbo wake 'Hallelujah'
aliowashirikisha Morgan Heritage ambao ulifikisha watazamaji Milioni 1 ndani ya saa 15 pekee.

HABARI HIZI ZINAPATIKA UDAKU SPECIAL APP BONYEZA HAPA UWE NAYO KWENYE SIMU YAKO

Loading...

WIMBO wa Tetema wa Rayvanny na Diamond yatoa Marekani WIMBO wa Tetema wa Rayvanny na Diamond yatoa Marekani Reviewed by Udaku Special on February 09, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.