Ajabu Atuma ujumbe kwa Vitendo kwa Kocha wa Taifa Stars

Kiungo wa timu ya Yanga SC, Ibrahim Ajibu ametuma ujumbe wa vitendo kwa Kocha wa Taifa Stars Emmanuel Amunike ikiwa zimebaki siku tisa kabla Taifa Stars haijacheza na Uganda kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza Kombe la Mataifa Afrika.

Mashabiki wa soka wamekuwa wakinung’unika chinichini kutokana na kocha wa Stars, Emmanuel Amunike kutomwita kiungo huyo kwenye timu ya taifa pamoja na kwamba amekuwa akifanya mambo makubwa uwanjani.

Ajibu wikiendi iliyopita alionyesha kuwa bado yupo kwenye chati baada ya kupiga pasi yake ya 15 ya bao kwa msimu huu baada ya kuiongoza timu yake kushinda kwa mabao 2-1 dhidi ya KMC. Huu ni ujumbe tosha kwa kocha huyo kuwa anakosea kutomjumuisha mchezaji huyo kwenye timu hiyo.

Mbali na huyo, pia Amunike ameshindwa kumuita kinara wa ufungaji kwenye ligi kwa sasa Salim Aiyee wa Mwadui ambaye amefunga mabao 15. Aiyee naye alimtumia ujumbe kocha huyo kwa kufunga bao moja wikiendi iliyopita baada ya timu yake kuifunga Mbeya City mabao 3-1.

HABARI HIZI ZINAPATIKA UDAKU SPECIAL APP BONYEZA HAPA UWE NAYO KWENYE SIMU YAKO

Loading...

Ajabu Atuma ujumbe kwa Vitendo kwa Kocha wa Taifa Stars Ajabu Atuma ujumbe kwa Vitendo kwa Kocha wa Taifa Stars Reviewed by Udaku Special on March 14, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.