Loading...

3/07/2019

Basi la Abood lakivaa kituo cha Mwendokasi

Basi la Abood lakivaa kituo cha Mwendokasi
Abiria waliokuwamo katika basi la Abood linalofanya safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro wamenusurika kufa baada ya basi hilo kuacha njia na kukigonga kituo cha mabasi yaendayo haraka kilichopo maeneo ya Kimara Corner wilayani Ubungo.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Mkuu wa operesheni wa kikosi cha usalama barabarani (Trafiki), Abdi Isango amesema ajali hiyo ilitokea leo Alhamis Machi 7,2019 saa 12: 30 asubuhi na chanzo chake ni mwendokasi wa dereva wa basi la Abood.

"Basi la Abood ambalo ni Marcopollo lilikuwa katika mwendokasi likikimbizana na basi lingine. Lilipofika maeneo hayo lilitaka kuovateki basi la mbele yake lakini kutokana kutokuwa makini wa kuacha nafasi alijikuta akiingia upande wa barabara ya mwendokasi na kuharibu miundombinu yake.

"Baada ya kuona nafasi ndogo kati ya basi jingine na ili asiligonge aliamua kuparamia barabara hiyo. Ameharibu nguzo za barabara hiyo na kituo pia gari lake kuharibika," amesema Isango.

Gari hilo limepelekwa katika Kituo cha Polisi Mbezi huku dereva wake akishikiliwa kwa mahojiano.
Loading...
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger