Kada wa CHADEMA amtetea Joshua Nassari kuvuliwa Ubunge


Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA)anazidi kugonga vichwa vya habari mara baada ya kuvuliwa Ubunge kutokana na kutohudhuria vikao vya Bunge.

Kada wa CHADEMA, Godlisen Malisa amemtetea Mbunge huyo kwa kueleza kuwa alikuwa akimuuguza mke wake kwa kipindi kirefu nchini Marekani. Chini ni kile alichoandika Malisa; 

Nimesikitishwa sana na kitendo cha Spika Ndugai kumvua ubunge, Mhe.Josh Nassari kwa madai ya utoro bungeni. Nassari amekuwa akimuuguza mkewe kwa muda sasa. Na kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake alilazimika kumpeleka Marekani kwa matibabu zaidi.

Kipindi chote hicho Nassari ndiye aliyekuwa akimhudumia mkewe hadi majuzi alipojifungua. Kutokana na umuhimu huo Nassari aliandika barua kwa Spika kutoa taarifa kuwa hataweza kuhudhuria vipindi kadhaa vya bunge hadi mkewe atakaporecorver.

Lakini Ndugai kamvua ubunge bila kujali yote hayo. Kanuni zinataka mbunge kutoa taarifa anaposhindwa kuhudhuria mikutano mitatu ya bunge. Nassari alitoa taarifa kwa mujibu wa kanuni. Mwisho wa kunukuu. 

Leo Spika wa Bunge amemvua ubunge Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA) kutokana na kutohudhuria vikao vya mikutano mitatu ya Bunge mfululizo (mkutano wa 12,13 na 14). Spika, Job Ndugai ameiandikia barua Tume ya Uchaguzi (NEC) kuitaarifa kuwa jimbo hilo lipo wazi.HABARI HIZI ZINAPATIKA UDAKU SPECIAL APP BONYEZA HAPA UWE NAYO KWENYE SIMU YAKO

Loading...

Kada wa CHADEMA amtetea Joshua Nassari kuvuliwa Ubunge Kada wa CHADEMA amtetea Joshua Nassari kuvuliwa Ubunge Reviewed by Udaku Special on March 14, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.