3/11/2019

Kichuya Mambo Magumu MISRI Timu Yake Yashikilia Mkia


TANGU kipenzi cha mashabiki wa Simba, Shiza Kichuya atue kwenye ardhi ya Misri hajawahi kushangilia ushindi na timu yake ya ENPPI.

 Tena mbaya zaidi ipo nafasi ya mwisho kabisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Misri. Kichuya alisajiliwa na Pharco Fc inayoshiriki Daraja la Pili ya Alexandria, Misri lakini ikampeleka ENPPI kwa mkopo mpaka msimu wa Ligi Kuu Misri umalizike.

 Mpaka sasa Kichuya amecheza mechi tatu akiwa anatoka au kuanzia benchi, amekosa mechi moja tu na tayari ana kadi moja ya njano. Katika mechi alizocheza ambazo ni dhidi ya Ahly walifungwa mabao 2-1, Zamalek ikawapiga 2-1 na Al Masry ikawala 3-1.

 Mechi ya wikiendi iliyopita ambayo ENPPI walilala mabao 2-1 Kichuya alikuwa benchi. Timu hiyo kwa sasa ni ya mwisho kwenye msimamo wa ligi ikiwa imecheza mechi 24 na kushinda nne tu tangu msimu uanze.

 Imepoteza michezo 11, ikatoka sare sita, imefungwa mabao 36 na kufunga 27 huku iking’ang’ania kwenye mstari wa kushuka daraja.

GPL
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger