No title

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwinyi Zahera aeleza Stars ilivyomkimbiza hotelini
Kocha wa timu ya Yanga ambaye pia ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya DR Congo, Mwinyi Zahera ameweka wazi kuwa baada ya mechi kati ya DR Congo na Liberia kumalizika, alitoka uwanjani na kukumbilia hotelini kutazama mechi ya Taifa Stars na Uganda.

Akiongea kwa simu na www.eatv.tv kutoka Kinshasa DR Congo, Zahera amesema jana ilikuwa ni siku ya furaha sana, haswa baada ya kushinda mchezo wao na Liberia na kufuzu AFCON 2019, kisha kuishuhudia Stars ikifuzu pia kwa kuifunga Uganda.

''Baada tu ya mchezo wetu nikamsubiri Rais Felix Tshisekedi, alipokuja kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kutupongeza lakini alipomaliza tu mimi nikakimbia hotelini kuingalia mechi ya Taifa Stars na nikakuta wanaongoza kwa bao 1-0 hivyo nikaona mabao mawili'', amesema.

Zahera pia ameeleza kuwa Taifa Stars walicheza mpira mzuri sana na kwa dakika chache tu, aliamini watashinda kwa mabao matatu na kweli wakafunga la pili kwa penati ambapo alishangilia kiasi cha wenzake kumshangaa sana haswa lilipoongezwa bao la tatu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad