Maajabu ya Ushindi wa Simba Kufuzu Robo Fainali

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


NDUGU yangu Francis Daud anasema kutokana na kutekwa na hisia za ushindi wa Simba dhidi ya AS Vita jana, kuna mtu alimuomba maji akambebea friji lote akampa.

Huyo anamzidi konda wa daladala Mbagala ambaye aliamua kugawa nauli kwa abiria badala ya kukusanya?

Nasikia Diamond baada ya ushindi alimpigia simu Ali Kiba akamshauri aachane na Coastal ajiunge na Simba ili amshangilie. Zari naye kwa furaha akampigia simu Diamond akamwambia: Simba ukuje South Africa, watoto wamekumiss.

Mmh! Zuwena alitoa kali jana? Alimkwida Kimpomo mbele ya mkewe, eti lazima wakalale wote. Akamuuliza: "Hii furaha ya Simba unataka niimalize vipi usiku huu nikiwa mwenyewe?" Mke wa Kimpomo akamwambia Kimpomo: Ushindi ni furaha. Na furaha huleta amani. Nenda tu na Zuwena mume wangu asubuhi utanikuta nyumbani.

Mishale ya saa 5 hivi, Kimpomo akapokea SMS ya mkewe: "Mume, kuna huyu jirani huwa nakwambia ananisumbuaga. Sijui amejua leo haupo? Kaja kuniganda hapa. Namfukuza haondoki." Kimpomo akamjibu: Mkaribishe tu ndani mke wangu. Leo ni furaha. Mpe fursa tufurahi pamoja.

Boss kubwa aliipa ofa ya uwanjani timu yake ya kazi. Usiku katikati ya sherehe, watu wake wakawa wanazungumza, mara Niyonzima hivi, ooh Niyonzima vile. Boss akawaambia: "Jamani hali ya biashara imekuwa ngumu. Mshahara wa Machi mtaupata Mei kama Simba atashinda fainali. Wafanyakazi wake wakashangilia: Bosi bosi bosi!

Rasta alimfuma Kipara akiwa na mkewe tangu Septemba 2016, na kuanzia hapo hawakuongea tena. Jana Kipara akapokea SMS kutoka kwa Rasta: Ndugu yangu, yaani tangu niwafume ndiyo umekata mawasiliano na waifu. Jah hapendi. Kama vipi leo aje kwako. One love!

Eti ni kweli Irene Uwoya alimtumia meseji Janjaro akamwambia amemmiss? Halafu Mobeto na Wema walipigiana simu na kukubaliana mmoja awe Tanzania Sweetheart na mwingine ni Naibu Tanzania Sweetheart?

Kimsingi ushindi wa Simba ni amani. Ni mapatano. Maadui wamekuwa marafiki. Wenye uhasama wamesameheana. Tunaomba Simba iendelee kushinda. Ushindi wa Simba ni suluhu ya chuki na magomvi.

Ndimi Luqman MALOTO
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad