3/18/2019

MARAIS Museveni na Kagame Hapatoshi, Watunishiana Misuli na Kuonyeshana Ubabe Live

Kwa taarifa za ndani kabisa nilizozipata ni kwamba huku Viongozi hawa waliokuwa Maswahiba ( Marafiki ) na wana Undugu pia wa Kikabila Rais Museveni na Rais Kagame wakiwa bado wanaendeleza Vita yao ya maneno hasa katika Mitandao yao ya ' Twitter ' tayari Vikosi vyao vya Kijeshi vimeanza Kusogezwa katika Mipaka yao na kwamba muda wowote kinaweza Kunuka ( Wakazichapa )


Rais Museveni jana wakati akiwaapisha Wapiganaji wa Vikosi huko Uganda alisema namnukuu...." Kuna Watu wanadhani Uganda ile waliyoizoea ndiyo hii kumbe wamesahau kuwa kila Siku Uganda inazidi Kuendelea na Kujizatiti halafu hatutishwi na wale wote wanaotujaribu na wasije Kuthubutu watajuta Kuifahamu Uganda ".

Rais Kagame nae juzi tu wakati akiwa katika Kongamano moja Jijini Kigali kama kawaida yake ' Mwanamume ' huyu wa Shoka kwa ' Kujiamini ' kabisa alisema namnukuu...
" Sijaanza Kuwindwa, Kuchukiwa, Kujaribiwa na hata Kutishwa na Wapuuuzi wachache na labda niwaambie tu kuwa Mimi sitokuja Kumpigia Magoti Mpuuzi yoyote kisha nimnyenyekee ila nitabaki kuwa Imara kama vile ambavyo nchi yangu ilivyo imara pamoja na Wananchi wake "

Kazi ipo!

Nawasilisha.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger