3/23/2019

Mchungaji Amuomba Rais Magufuli Kumjengea KanisaNa. John Walter,Babati

Mchungaji Emmanueli wa kanisa  la Jesus Life Assemblies  lililopo kitongoji cha Qatabradik  anayeshutumiwa  kutumia  nguvu za Free Mason amemuomba Rais John  Magufuli kumsaidia kujenga kanisa  na waumini wamemkingia  kifua  wakikanusha tuhuma hizo.

Ombi  hilo alilitoa mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na Nipashe  eneo ambalo anatoa huduma ya kiroho  ya kuombea watu na kuubili  katika jirani na barabara ambapo anadai ameomba kwa muumini wake.

Mchungaji Tsino alisema kuwa  yeye hatumii nguvu  za free mason kama watu wa jamii  ya pale  wanavyosema  badala yake anadai  anatumia  eneo la mungu ambalo limekuwepo siku zote  hivyo  hana chochote anachokitumia.

“Ninamuomba Rais wangu  John Magufuli  anisaidie kupata eneo la kujenga kanisa  na anisaidie kujenga  ili niendelee  kumuombea na kuwaombea watu wengine  ambao wana shida  kama  ambavyo nafanya  hapa,’’Alisema Tsino

Aidha alisema  toka  aanzishe huduma hiyo  kumekuwepo na maneno  ya kumpiga  kashfa  kua ni free mason  ila yeye anasema  aliamua kufikisha injili  maeneo ya vijijini ambako watumishi wengi wa mungu hawafiki  ili watu wa vijijini waweze kusaidika.

Mmoja wa waumini wake Lucy Peter akizungumza na Nipashe alipinga mchungaji huyo kutumia nguvu za free mason  huku akidai alifika kanisani hapo alikua  amepooza ulimi  na mikono alimuombea bila kutumia kitu chochote na alipona  na mpaka sasa anaendelea na shughuli zake.

 Beatha Pius  naye ni muumini wa kanisa hilo ambaye amemkingia kifua mchungaji huyo na  kukanusha tuhuma za free mason  anazoshutumiwa mchungaji  wake huku akisema alimuombea akapona ugonjwa wa kifua aliokua amezunguka  Hospitali nyingi bila mafanikio  na anampongeza amewaombea vijana wameacha pombe.

Mzee Tsolo Fisoo alisema mchungaji huyo anawaombea watu wengi wanapona  na vijana wameanza kubadirika ila kusema ni Free Mason hizo ni fitina za watu wa madhebu mengine  wanaolenga  mkufitini asiendelee.

Naye mwenyekiti wa kitongoji cha Qatabradik Rubanus Slaa alisema wao kama serikali wamempokea vizuri akiwa na vielelezo vyote vya usajili wa kanisa  lake huku akisema huduma anayoifanya inaisaidia serikali kukomesha vitendo vya kiharifu  na akadai amewabadirisha  vijana waliokuwa walevi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger