Loading...

3/07/2019

Nandy azua gumzo mtandaoni na ujumbe ulioambatana na video ya Ruge

Nandy azua gumzo mtandaoni na ujumbe ulioambatana na video ya Ruge
Baada ya ukimya wa muda mrefu Nandy ‘African Princess’ amevunja ukimya na kumzunguzia Ruge Mutahaba kwa kuandika ujumbe katika ukurasa wake wa Instagram huku akiambatanisha na video ambayo imezua gunzo mtandaoni.


Msanii huyo  kipindi chote cha msiba aligusa hisia za wengi kutokana na namna alivyoonekana  wakati wote akiwa sehemu ya familia ya Ruge jambo lililoibua maswali kuhusu uhusiano wake na marehemu.

Katika ujumbe wake Nandy amemuelezea Ruge kama rafiki yake wa karibu aliyeelewa ndoto zake na kumpa moyo wa kupambana.

View this post on Instagram
Nandy avunja ukimya na video ya Ruge #Repost @officialnandy (@get_repost) ・・・ Kila mtu ana mtu ambaye ameumbwa na MUNGU kwa ajili yake. Na jinsi yakukutana na uyo mtu inaweza ikawa ni ndefu ikawa na matuta mara nyingine inaweza ikakuchosha lakini mwisho wa siku kila kitu kinakuja kuwa sawa.. Wanaweza kutokea watu wachache ambao watakuelewa na pia kuelewa ndoto zako hata kama unazifanya mwenyewe.. watakuwa hapo kukupa mrejesho chanya na watakubeba kwenye safari yako kwa moyo wote… Watanzania wanakupenda Umegusa maisha ya watu kwa namna tofauti tofauti Ulizaliwa kuwa kiongozi Ulikuwa na moyo wakutoa.. Ruge ulikuwa rafiki yangu wa karibu sana, ulikuwa kila kitu kwangu Ruge ulielewa ndoto yangu Ruge ulinipa moyo wa kupambana hata kama nilikua nataka ku give up Ruge uliona ndoto yangu na hukuwa na wasiwasi nayo…. Ulivo pumzika naweza kukuhakikishia… Nitakufanya ujivunie… Nitaendelea kuzi enzi na kuziishi hekima zako Na nitafanya juhudi kufikia malengo tuliyo panga pamoja.. Nakupenda sana na nitaendelea kukupenda hata kama haupo nasi YOUR THE BEST THING THAT EVER HAPPEN TO ME ROHO YANGU.. R.I.P

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on Mar 6, 2019 at 8:27am PST

Ujumbe huo uliokwenda sambamba na video inayomuonyesha Ruge akicheza na mbwa unasomeka: “ Kila mtu ana mtu ambaye ameumbwa na Mungu kwa ajili yake, jinsi ya kukutana na huyo mtu inaweza ikawa safari ni ndefu, ikawa na matuta na mara nyingine inaweza ikachosha lakini mwisho wa siku kila kitu kinakuja kuwa sawa.

“Wanaweza kutokea wachache ambao watakuelewa na pia kuelewa ndoto zako hata kama unazifanya mwenyewe. Watanzania wanakupenda umegusa maisha yao kwa namna tofauti ulizaliwa kuwa kiongozi, ulikuwa na moyo wa kutoa.”

Ameendelea kumuelezea Ruge akisema: Ulikuwa rafiki yangu wa karibu sana, ulikuwa kila kitu kwangu. Ruge ulielewa ndoto yangu na ulinipa moyo wa kupambana hata kama nilikuwa nataka kukata tamaa.”

“Nakuhakikishia nitakufanya ujivunie, nitaendelea kuzienzi na kuziishi hekima zako na nitafanya juhudi kufikia malengo tuliyopanga pamoja. Nakupenda sana na nitaendelea kukupenda hata kama haupo nasi.

Related Articles

Ommy Dimpoz aonyesha Show yake ya kwanza kuifanya Muscat wakati akitest Voko lake kama lipo fiti (+ Video)
 23 hours ago

Baada ya kukumbwa na sakata la kuwalawiti watoto wadogo, Michael Jackson zaidi ya vituo 23 vya Radio kutoka nchi tofauti, vimesitisha kucheza nyimbo zake
 1 day ago

R.Kelly alia kwenye mahojiano akisisitiza anaonewa, mashitaka yote 10 ya kuwarubuni wasichana wadogo kingono sio ya kweli (+Video)
 1 day ago

Mama Ruge: Afadhali Ruge ametuachia watoto, asingekuwa na watoto tungeumia zaidi (Video)
 1 day ago
Habari Zinazotrend

Zari Hassan’s emotional message to Diamond
 July 23, 2018 - 5:30 pm

Wimbo mpya wa ‘Happy’ wa Rich Mavoko waibua mapya, mashabiki wake wampongeza kuondoka WCB
 July 23, 2018 - 2:14 pm

Fahamu ugonjwa unaomsumbua Ommy Dimpoz, mtaalamu wa afya aeleza vyanzo vyake na kutoa tahadhari kwa wasanii (+Audio)
 July 20, 2018 - 6:14 pm

Posti ya Harmonize aliyomuweka Harmorapa na Harmo Junior mtandaoni yamchanganya msanii mkubwa barani Afrika
 July 24, 2018 - 1:40 pm

Zari awapiga STOP Wema na Aunty Ezekiel kwenda Afrika Kusini kwenye Birthday ya Tiffah ‘mtanichafulia nyumba yangu’
 July 26, 2018 - 1:50 pmHabari zilizopita
 Habari zilizopita
© Copyright 2019, All Rights Reserved  |  Bongo5 Media Group, powered by Wordpress.

Loading...
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger