4/15/2019

Asakwa na polisi baada ya kudukua mtandao wa Serikali na kujiajiri


Polisi Nchini Afrika Kusini wanamsaka kijana aliyedukua na kujiajiri kwenye sekta ya Afya na kisha kujilipa mshahara.

Bright Chabola aliyesomea ‘Computer Engineering’ alidukua mtandao wa Serikali na kujiajiri Upande wa Afya kama Msimamizi wa Mfumo mwaka 2018.

Kijana huyo aliwambia wazazi wake kuwa amepata kazi nzuri na analipwa mshahara Randi 7000(zaidi ya shilingi 1,100,000 za Kitanzania).

Kijana huyo alijulikana kufanya kosa hilo baada ya kuonekana anapokea mshahara bila kulipa kodi na alipofatiliwa na kugundulika kuwa hata kazini alikuwa haendi na ameanza kupokea mshahara tangu mwezi Juni, mwaka 2018.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger