4/17/2019

Blac Chyna Kufunguliwa Mashtaka Kisa kodi ya Nyumba

Blac Chyna Kufunguliwa Mashtaka  Kisa kodi ya Nyumba
Mtandao wa The Blast umeripoti kuwa  Blac Chyna afunguliwa mashtaka na mwenye nyumba wake baada ya kushindwa kukamilisha kodi ya nyumba aliyoipanga na hivyo kudaiwa jumla ya kiasi cha dola za kimarekani $48,000 sawa na zaidi ya shilingi Milioni 100 za Kitanzania.

Kwa mujibu wa nyaraka za Mahakama  zinaripoti kuwa Michael Kremerman ambaye ni mwenye nyumba amefungua mashtaka na kudai kuwa mwaka 2017 Blac Chyna aliingia mkataba wa kuishi kwa mwaka mmoja kwenye nyumba ya vyumba sita, mabafu matano ikiwa na studio ambapo nyumba hiyo iligharimu dola za kimarekani $16,000 sawa na zaidi ya shilingi Milioni 37 za Kitanzania kodi ya mwezi.

Michael Kremerman aliendelea na kudai kuwa Chyna aliongeza mkataba hadi March 31, 2019   lakini ilipofika November 2018 alihama hivyo miezi yote iliyobaki ili kukamilisha mkataba hakuwa analipa kodi hivyo Kremerman alisema anamdai jumla ya kiasi cha dola za Kimarekani $48,552 sawa na zaidi ya Mil. 112 za Kitanzania ukimjulisha na pesa za uharibifu alioufanya ndani ya nyumba hiyo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger