4/10/2019

Dismas Ten Amkaribisha Mwekezaji wa Bilioni 120

Dismas Ten Amkaribisha Mwekezaji wa Bilioni 120
Afisa habari wa Yanga, Dismas Ten amewatupia dongo jipya watani wao wa jadi Simba baada ya kutaja thamani ya klabu hiyo.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Dismas Ten ameandika kuwa baada ya uchaguzi kupita, klabu hiyo itaingia katika uwekezaji mkubwa huku akitaja thamani ya klabu hiyo kuwa ni takribani bilioni 120.

"Kwa kuwa umekubali acha nikustue jambo. Kwa mujibu wa taarifa na hesabu zilizopo mezani, thamani ya Yanga ni Tsh bilioni 120 (Mara ya sita ya thamani ya Simba) ikiwa na gawanyo la bilioni 30 kwa Kila miezi 3 katika miezi 12 inaunda mwaka mzima", amesema Dismas.

"Anyway kwenye hili najua wengi hawataelewa, wachache wataelewa ukiwemo wewe kwa sababu ni mfanyabiashara mwenye akili kubwa, najua utashtuka kidogo but ndo ‘nshakusanua mtindo’. Acha tusubiri uchaguzi upite, karibu sana YANGA SC ila 'please' ujumbe kwenye bango uuchukulie kwa uzito wa juu..!", ameongeza.

Yanga itaingia katika uchaguzi mkuu mnamo mwezi ujao, ikiwa ni baada ya kusuasua kwa taratibu za uchaguzi wa awali zilizokuwa zikisimamiwa na TFF.

Ikumbukwe kuwa Simba iliingia katika mfumo wa mabadiliko, baada ya mwekezaji Mohamed Dewji 'Mo' kujitokeza na kuweka kiasi cha bilioni 20 ambazo zilikwenda sambamba na hisa za asilimia 49.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger