4/15/2019

Hamisa Mobetto Apooza Machungu ya Manara


Msemaji wa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania, Haji Sunday Manara, amemshukuru mwanamitindo na msanii wa kizazi kipya nchini, Hamisa Mobetto kwa kufanikiwa kumpooza maumivu baada ya jana Simba kutolewa nje ya michuano ya mabingwa Afrika.

Simba jana walitolewa rasmi katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kukubali kichapo ugenini cha goli 4-1 dhidi ya TP Mazembe.

Manara ameeleza kwamba Hamisa ni walioamua kupooza machungu yake kwa kqwenda kutazama naye mechi nyumbani kwake hata kumfariji baada ya matokeo mabaya.

Manara ameongeza kwamba kwa kitendo alichokifanya mwanadada huyo anapaswa kufahamu kwamba anampenda sana na afahamu kuwa ana thamani kubwa kwake.

Mbali na hayo Manara ameongeza kwamba, "Tumetolewa lakini tumeacha alama, tusijilaumu bali kwa hatua hii tujipongeze na Inshaallah Mwakani tutarudi kwa nguvu kubwa Kwenye Ligi ya Mabingwa"

"Sasa tunarudi kwa nguvu kubwa kuchukua ubingwa wetu wa Tanzania" amesisistiza
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger