4/16/2019

Lembeli Atoboa Siri kuhama CHADEMA, Amtaja Rais Magufuli

Lembeli Atoboa Siri kuhama CHADEMA, Amtaja Rais Magufuli
Mbunge wa zamani wa Kahama, James Lembeli amesema alihamia CHADEMA kujibanza tu ila kurudi CCM kulitokana na kushauri na Rais Magufuli na familia yake.

Akizungumza kwenye kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV amesema kuwa tangu aliporejea CCM amekuwa mtu mwenye amani na furaha.

"Rais Dkt. John Magufuli alikuwa kwenye ziara Kahama nilikwenda kwenye mkutano wake wananchi wakaniambia nirudi nyumbani, lakini pia Rais aliniambia nirudi tuijenge Tanzania, nikaamua kurudi, nilikwenda CHADEMA kujibanza kwenye mvua," amesema.

Amendelea kwa kusema, 'Mama yangu anaheshimika sana, kuhama kwangu CCM ilimkwaza sana aliniambia chama ambacho baba yako alikipigania wewe umeondoka, akaniambia nirudi kwa sasa nina amani na furaha,'.

Alipoulizwa ni kwanini kwa sasa hivi amekuwa kimya kwenye siasa za Tanzania, alijibu, 'Nimekuwa kimya kwa sababu za harakati za maisha zamani ilikuwa rahisi kuniona kwa sababu nilikuwa kwenye siasa kwa sasa nipo Kahama nafanya shughuli zangu" James Lembeli, Mbunge wa zamani wa Kahama'.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger