4/15/2019

Mbwana Samatta Azidi Kutisha KRC Genk

Mbwana Samatta azidi kutisha KRC Genk
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku huu amesababisha bao la pili na kufunga la tatu kuisaidia timu yake, KRC Genk kuibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Club Brugge katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.

Leandro Trossard alifunga bao la kwanza dakika ya 13, kabla ya H. Vanaken kuisawazishia Club Brugge kwa penalti dakika ya 36. Mbwana Samatta akapiga shuti likambabatiza beki wa Club Brugge na Ruslan Malinovskiy akaenda kufunga kwa penalti dakika ya 55.

Samatta mwenye umri wa miaka 26, usiku huu amecheza mechi ya 150 kwenye mashindano yote na akiwa amefunga mabao 60 tangu amejiunga na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger