4/20/2019

Nicki Minaj Aachana na Menejimenti Yake

RAPA Nicki Minaj ameachana na menejimenti yake YA  Blueprint/Maverick Gee Roberson kwa madai kwamba amekuwa akifanya kazi na watu watatu kwa mkupuo, jambo linaloweza kuwa linasumbua.

Chanzo kimoja kimeelezakuwa maamuzi hayo yalikuwa ya kawaida tu na hakukuwa na sababu rasmi ya kuvunjika kwa ushirikiano wao. Hii imekuja baada ya Nicki kuandamwa na matatizo kadhaa ya kiufundi  kwenye steji ambapo wiki iliyopita alipata tatizo la sauti kwenye shoo iliyofanywa na  Coachella akishirikiana na Ariana Grande. Tatizo  hilo limekuwa sugu kwani miezi kadhaa nyuma lilimwandama na kulazimu kusogeza shoo mbele.


Hilo ni moja ya matatizo mengi yanayomwandama Nicki tangu mgogoro wa kuachia albam yake ya Queen mnamo Agosti 2018, mbali ugonvi wake na mwanamuziki Cardi B.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger