4/15/2019

Rais wa Misri Akutana na Haftar wa Libya

Rais wa Misri akutana na Haftar wa Libya
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amekutana leo na jenerali muasi wa Libya Khalifa Haftar, ambaye vikosi vyake vinapambana kutaka kuudhibiti mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli.

Taarifa ya Ikulu ya Misri imesema Sisi amesema anaunga mkono jitihada za kupambana na ugaidi na makundi ya wanamgambo yenye misimamo mikali ili wananchi wa Libya wawe na usalama na utulivu nchini kote.

Sisi amekuwa mshirika mkuu wa vikosi vya Haftar, ambavyo vinadhibiti maeneo makubwa ya mashariki mwa Libya na mnamo Aprili 5 vilianzisha mashambulizi ya kutaka kuudhibiti mji mkuu wa Tripoli.

Mapigano hayo ya nchini Libya yameripotiwa na Shirika la Afya Duniani WHO kusababisha vifo vya watu 121 na wengine 561 kujeruhiwa.

 Haftar ametupilia mbali wito wa kimataifa unaomtaka asitishe mapigano dhidi ya wapiganaji tiifu kwa serikali ya Libya yenye makao yake mjini Tripoli na inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger