Ray Afunguka Kuhusu Mpenzi Wake Mpya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ray afunguka kuhusu mpenzi wake mpya
Msanii wa kiume wa filamu bongo, Vicent Kigosi maarufu kama Ray, amefunguka juu ya madai ya kuachana na mama mtoto wake Chuchu Hans na kuwa na mahusiano mapya na msanii Sarafina.


Akizungumzia hilo Ray amesema kwamba hawezi kuzuia watu kuongea, lakini ameamua kuachana nao huku akiangalia zaidi mustakabali wa maisha yake.

“Mimi nawaangalia tu watu wavyosema hovyo. Mara sijui nilikuwa na Tessy, mara Fina (Sarafina) sasa mimi nawaacha wenyewe watajua na kuhukumu wajuavyo, naendelea na mambo yangu,” amesema Ray.

Hata hivyo mama mtoto wake Chuchu Hans amesema kwamba kwa sasa hana muda wa kumfuatilia Ray kwani kama ameshaamua kufanya hivyo hawezi mzuia, na ameshazoea kuumizwa kwenye mahusiano, “unajua kuna wakati mtu unaishiwa hata maneno ya kusema, halafu kingine sina muda tena wa kumfuatilia mtu na kama kaamua hivyo sawa ni kwa faida yake maana wengine tushazoea kuumizwa siku zote”, amema Chuchu Hans.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa wawili hao hawapo pamoja tena, huku Ray akitajwa kuwa kwenye mahusiano mapya na muigizaji wa bongo movie, Sarafina.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad