Spika Ndugai Amvaa Tena CAG Professa Assad, Asema Anampa Wakati Mgumu sana Rais

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema kitendo cha Mdhibiti Mkuu na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad kuendelea kuwepo ofisini mpaka sasa ni kumpa rais wakati mgumu kwa kuwa wao bunge wameshaeleza kuwa hawamtaki


Ndugai ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabaji Jijini Dodoma ambapo amesema kwamba kwa kitendo cha Bunge kumkataa Prof Assad alipaswa ajiongeze kwa kujiuzulu.

"Tunataka tumuoneshe Prof. Assad kuwa Bunge halichezewi, simuelekezi kazi  ila anatakiwa ajiongeze kama ni kujiuzulu au la! maana tushamwambia  hatumtaki, anavyoendelea kubaki ofisini ni kumpa tu wakati mgumu Rais.
 
 "Sisi kama Bunge hatutaki hilo neno dhaifu, kwa sababu Bunge kama Bunge  halifanyiwi tathmini na ofisi ya CAG ila wanaofanyiwa tathmini ni  watendaji wa Ofisi hiyo hivyo hawakupaswa kudhihakiwa na lugha hiyo  inayotajwa kuwa ya kihasibu".

Aidha kuonyeshwa kukerwa na neno 'Dhaifu analoendelea kulitumia Prof Assad, Ndugai amesema kwamba  kama yeye analipenda sana neno hilo ajiite na kwamba wao kama bunge wameikataa na hawalipendi.

Kuhusu kazi za CAG, Spika amefafanua kwamba; "Hatuna tatizo na ripoti ya CAG…tatizo letu ni maneno ambayo Prof. Assad ameyatoa akiwa Marekani, na alipoita waandishi akarudia  tena, maneno yale sie tumeyakataa sio ya kistaarabu.

Spika Ndugai amemsifu Profesa Assad kwa ujasiri wake huku akiufananisha na ujasiri wa mbwa kumtukana mtu anayemlisha.

"Unatukana hadi mkono unaokulisha, inahitaji ujasiri na jamaa ana ujasiri. Ila ni ujasiri ule wa mbwa anayemtukana anayemlisha," amesema.

Hata hivyo, Ndugai amesema hana chuki binafsi na Assad bali tatizo ni lugha tu aliyotumia ya kuliita Bunge dhaifu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad