Umoja wa Mataifa Walaani Mauaji Saudia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Umoja wa Mataifa Walaani Mauaji Saudia
Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kutetea haki za binadamu Michelle Bachelet ameilaani vikali hatua ya Saudi Arabia ya kutekeleza hukumu za kifo.

Saudia ilitekeleza jambo hilo kwa kuwakata vichwa watu 37 katika miji sita nchini humo, Wizara ya usalama wa ndani ya Saudia ilisema watu hao ambao wote ni raia wa Saudi Arabia walinyongwa kwa kuhusishwa na ugaidi.

Na sasa Bachelet amesema anasikitishwa kwa kutofuatwa kwa sheria na utaratibu wa kimahakama kutokana na madai kuwa washukiwa walikiri kujihusisha na ugaidi baada ya kuteswa.

Ameutaka uongozi wa Saudi Arabia kuangazia upya sheria za kupambana na ugaidi na kusimamisha mauaji yaliyokuwa yamepangiwa kufanywa, yakiwemo ya watu watatu ambao bado wanakabiliwa na hukumu ya kifo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad