4/16/2019

Wasiojulikana Waibuka Mkoani Kilimanjaro, Waua Watu Watatu Kikatili Akiwemo Mtoto wa Miaka 8

Wasiojulikana Waibuka Mkoani Kilimanjaro, Waua Watu Watatu Kikatili Akiwemo Mtoto wa Miaka 8
Watu watatu wameuwawa kikatili mkoani Kilimanjaro akiwamo mtoto wa miaka 8 kuuwawa kwa kukatwa katwa kwa mapanga na watu wasiojulikana.

Kamanda wa PolisI mkoani Kilimanjaro, Hamis Issah
Akithibitisha tukio hilo jana Aprili 15, Kamanda wa PolisI mkoani humo Hamis Issah amesema tukio la mtoto kukatwa mapanga lilitokea april 14 mwaka huu.

Amesema mtoto huyo akiwa amelela na mama yake watu wasiojulikana walimvamia na kumkata mapanga shingoni na mkono wa kulia.

“Mtoto Sarafina Williamu (8) ambaye alikuwa mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Mavula, kabla ya kifo chake alifanyiwa tukio la udhalilishaji ambapo kesi hiyo ilitolewa hukumu,”amesema Kamanda Issah.

Katika tukio lingine mama na mtoto wake wameuwawa kwa kunyongwa hadi kufa na watu wasiojulikana.

Kamanda Issah amesema tukio hilo lilitokea April 13 mwaka huu, mama huyo Koini Molell(70) na mtoto wake Sondoo Karika(30)wamekutwa wakiwa wemnyongwa hadi kufa ambapo kijana huyo alikutwa na kamba shingoni na mama yake shingo ikiwa imelegea.

“Uchunguzi wa awali uliofanywa na Jeshi la Polisi umebaini mauaji hayo yamefanywa kutokana na visasi na kwamba uchunguzi unaendelea ili kuweza kubaini ukweli na watuhumiwa kufikishwa kwenye vyomba vya sheria,” amesema Kamanda Issah.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger