Alikiba na Mbwana Samatta Wazungumzia Mchezo Wao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Alikiba na Mbwana Samatta Wazungumzia Mchezo Wao
Naohodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta amesema ktk mchezo wa kirafiki utakaowakutanisha Team Kiba na Samatta June 02, 2019 watu wenye ulemavu wataingia uwanjani bure na wataangalia namna ya kuisaidia timu ya Taifa ya watu wenye ulemavu.

Akizungumza leo na Waandishi wa Habari, Mbwana Samatta amesema ni jambo jema kama Watanzania kusaidiana na uchangiaji wa mambo ya kijamii hasa katika elimu usiishie siku ya mchezo huo pekee.

Kwa upande wake Alikiba amesema kuwa, "Mimi na Samatta hatujawahi kukaa na kuzungumza mambo ya kuisaidia jamii, lakini siku zote mtu mwema anakutana na mtu mwema na tulivyoanza tulianza katika kama utani lakini leo hii imekuwa kitu kikubwa" .

Ameendelea kwa kusema, "Sisi kama SAMAKIBA Foundation tulianzisha taasisi hii kwaajili ya kusaidia jamii, wengi wanaweza kuisaidia jamii lakini ni lazima uwe na huo moyo wa kusaidia".
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad