BREAKING : Mtu mmoja afariki dunia na 15 wajeruhiwa katika ajali ya basi na lori

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 15 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la New Force lililogongana na lori kati ya eneo la Mafinga na Nyololo mkoani Iringa.

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamhuri William amesema ajali hiyo imetokea kwenye misitu ya Sao Hill, na dereva wa lori amefariki dunia papo hapo.



Ajali hiyo imehusisha basi la New Force lililokuwa likitoka jijini Dar es Salaam kwenda Jijini Mbeya na liligongana na lori hilo lililokuwa limeingia ghafla barabarani likitokea kwenye barabara ya mchepuko.

“Bado tunaendelea kuchambua idadi ya majeruhi lakini hadi sasa aliyefariki dunia  katika ajali hiyo ni mtu mmoja ambaye ni dereva wa lori lililohusika kwenye ajali hiyo, idadi ya majeruhi hadi sasa ni 15,” amesema mkuu huyo wa wilaya.

Amesema baadhi ya majeruhi wamepelekwa hospitali ya Mafinga kwa matibabu kutokana na majeraha waliyopata kwenye ajali hiyo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad