5/12/2019

Kimenuka..Watu Wawili Washikiliwa na Jeshi la Polisi Kwa Kuiba Vito vya Dhahabu Nyumbani Kwa MengiWatu wasiofahamika wameiba vito, vifaa vya thamani na fedha taslimu katika nyumba ya mjane, Jacqueline Mengi na nyumba familia ambapo Dkt. Reginald Mengi alizikwa. Vitu vilivyoibwa ni mikufu ya dhahabu, 'laptop,' na fedha taslimu, mali ya familia na waombolezaji.

Msemaji wa familia hiyo Benson Mengi amesema kwa sasa hawawezi kuzungumzia jambo hilo kwa kuwa bado uchunguzi unaendelea.

Kwa upande wake Kamanda wa polisi mkoa Kilimanjaro, Hamis Issah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la wizi kwenye nyumba za kifahari za marehemu Mengi na amedai kuwa tukio hilo limefanyika na watu wanaodaiwa kuwa wa ndani ya familia kwani taarifa zinazonyesha walitokea jijini Dar es salaam.

”Ni kweli nyumbani kwa Mengi kumeibiwa amesema Kamanda” amesema Kamanda.

Hata hivyo tayari jeshi la polisi linawashikilia watu wawili ambao majina yao hayakuwekwa wazi wakidaiwa kuhusika na tukio hilo la wizi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger