5/12/2019

Manchester City yaitoa machozi Liverpool..Yachukua Ubingwa Ligi Kuu ya UingerezaKlabu ya Manchester City imefanikiwa kuunyakua Ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuilaza Brighton and Hove Albion mabao 4-1.

Katika mchezo huo ambao City ilikua ugenini ilitanguliwa kufungwa, ambapo Glenn Murray aliweza kuipatia bao Brighton and Hove Albion dakika ya 27 lakini  Sergio Aguero alisawazishia City dakika ya 28 na magoli mengine yalifunwa na  Aymeric Laporte dakika ya 38,  Riyad Mahrez dakika ya 63 na la mwisho likifungwa na Ilkay Gundogan dakika ya 72.

Kwa ushindi huo City imeweza kufikisha alama 98 na kujinyakulia Ubingwa huo ambao ilikua ikikimbizana na Liverpool ambayo imefikisha alama 97.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger