Membe: Mimi na Rostam ni Watoto wa Kambo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika awamu ya nne, Bernard Membe, amesema yeye na rafiki yake Rostam Aziz ni miongoni mwa watu ambao wanakasoro kwa kutumia kauli kuwa wamekatwa mkia bila ya kufafanua chochote.

Membe ametoa kauli hiyo akiwa nje ya jengo la Mahakama kuu ya Tanzania, wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka kusikilizwa kwa kesi anayodai fidia dhidi ya mmiliki wa gazeti la Tanzanite Cyprian Musiba, ambapo aliulizwa swali kuhusiana na kauli inayodaiwa kutolewa na mfanyabiashara Rostam Aziz kuhusiana na uchaguzi wa mwakani.

Membe amesema kuwa "kuhusu kugombea mwakani napata kigugumizi kumjibu Rostam, lakini yeye ni mchumi na nitakutana naye nimshauri anafanya vizuri kwa Watanzania anapozungumzia masuala ya uchumi, inabidi azungumzie 'main issue' za nchi sio 'personal', hizi tunaachia watu wa chini."

"Kwa 'level' yetu ni kuzungumzia masuala ya kitaifa masuala ya kiuchumi, kwanini uchumi wetu hapa ulipo? kwanini wafanyabiashara wanafunga biashara zao, Rostam ni 'economist' namshauri ajiadress kwenye masuala ya kiuchumi, Rostam wewe ni mwenzetu sisi tumekatwa mkia." amesema Membe.

"Ukikatwa mkia hata ujitahidi vipi mkia wako ni mfupi tu, tunayoyazungumza ni vizuri tuwe 'consistency' mdomoni na dhamira yetu, Rostam ni mchumi mzuri sana, tuzungumzie masuala ya uchumi wa nchi yetu, kuliko kujaribu kuwa mtoto mzawa badala ya kukubali 'status' Rostam na mimi ni watoto wa kambo." alimaliza Membe.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad