5/17/2019

Moi Atakiwa Kulipa Ksh Bilioni 1.6 Kwa Kunyakua Shamba la Mjane


Rais mstaafu wa Kenya, Daniel Arap Moi ameamriwa na Mahakama Kuu jijini Nairobi amlipe fidia ya Ksh. bilioni 1.6 Susan Cheburet Chelungui na mwanawe David Chelungui kwa kosa la kutumia mamlaka yake vibaya na kuwanyang'anya shamba familia hiyo mnamo mwaka 1983

Mjane huyo aliporwa shamba lake kwa njia ya udanganyifu huku maafisa wakuu Serikalini wakitumiwa katika udanganyifu huo na kisha kuliuza shamba hilo kwa kampuni ya Rai Plywood (K) Limited

Mahakama ilisema kuwa mbali na Rais Moi, sehemu ya shamba hilo pia iligawiwa kwa aliyekuwa Waziri msaidizi kwenye utawala wa Moi, Stanley Metto

Jaji Ombwayo alisema hakukuwa na ushahidi wowote kuonesha uhalali wa Rais huyo mstaafu kusajiliwa kama mmiliki halali wa shamba hilo  - #regrann
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger