5/12/2019

Ndege ya abiria yatua kwa dharura kwa kutumia matairi yake ya nyuma tuNdege ya abiria  imeripotiwa kutua  kwa dharura kwa kutumia matairi yake ya nyuma tu katika uwanja wa ndege nchini Myanmar.

Kwa mujibu wa Miami Herald, ndege ya Embaer-190 kutoka shirika la ndege la Myanmar ililazimika kutua lwa dharura katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mandalay kwa kutumia matairi yake ya nyuma tu kutokana na kutofunguliwa kwa matairi yake ya mbele.

Cheche za moto zilizonekana wakati wa kutua kwa ndege hiyo.

Msemaji wa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mandalay Kyaw San,amesema abiria 82 na wafanyakazi wa ndege kutoka Yangon, hawakujeruhiwa wakati wa kutua.

Kulinga na Kyaw San ndege za Boeing na Airbus hazitatumika katika uwanja huo wa ndege kwa muda mfupi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger