Nikki wa Pili akosoa maneno matakatifu ya Mungu juu ya uumbaji wa mwanamke, Kikwete na Billnass wamtolea povu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nikki wa Pili ametoa maoni hayo kwenye mitandao ya kijamii kwa kusema kuwa sio kweli mwanaume alikuwa wa kwanza kuumbwa na Mungu kama Biblia inavyoeleza, bali mfumo wa zamani ulikuwa mfumo dume na Biblia iliandikwa na wanaume.

“Stori inayosema Mungu alimuumba kwanza mwanaume, alafu baadae akaja kumuumba mwanamke kutoka mbavu zake, nadhani iko hivyo kwa sababu imeandikwa na mwanaume na iliandikwa kipindi ambacho jamii zilikua nyuma sana katika haki za kijinsia, ni Stori ya kimfumo dume,“ameandika Nikki wa Pili.

Maoni hayo yalipokelewa tofauti kabisa na mashabiki wake pamoja na wasanii wenzake akiwemo Billnass ambaye alimwambia kuwa amefikia hatua ya  kukosoa Biblia kisa kuoa mwanamke mzuri.

“Tumefikia Kukosoa Bible Kweli Nickson ? Inawezekana Mtu Ukipata Mwanamke Mzuri unaweza kusema Chochote,juu ya chochote bila kumhofia yeyote,” ameandika Billnass .

Mwingine aliyejitokeza kumshauri ni Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete ambaye ambaye amemwambia atafakari kwa kina kwani maneno yaliyoandikwa ni matakatifu na ukweli utabaki kuwa hivyo.

“Nikuombe umuogope Mungu. Hizo ni hadithi takatifu na ndiyo ukweli. Maana tunakoelekea mtakuja kututhibishia kuwa Tulianza kama nyani na kuwa Evolution is Really. Nadhani hilo ni tatizo. Mengine haya ni ya Mwenyezo Mungu, anataka kutuambia kuwa Mungu anajinsi ya Me,” ametoa ushauri Ridhiwani Kikwete .

Hata hivyo watu wengi waliotoa maoni yao wameoneshwa kukerwa na Nikki wa Pili juu ya mtazamo wake huo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad